Mpanda FM

Mama atupa kichanga kichakani Mpanda

12 February 2024, 9:00 am

Wananchi wa mtaa huo wameonesha kusikitishwa na tukio hilo huku wakiomba sheria ichukue mkondo wake” Picha na Ben Gadau

Na Ben Gadau-Katavi

Mtoto mchanga wa umri wa siku moja amekutwa ametupwa katika mtaa wa mlimani site kata ya Uwanja wa ndege manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Wakizungumza na kituo hiki katika eneo la tukio baadhi ya wananchi wa mtaa huo wameonyesha kusikitishwa na tukio hilo huku wakiomba sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa wakitekeleza matukio ya aina hiyo.

Sauti za wananchi wa mtaa wa mlimani site kata ya uwanja wa ndege wakielezea kusikitishwa na tukio hilo.

Wananchi wa mtaa wa mlimani site kata ya Uwanja wa ndege wakiwa eneo hilo ambalo mtoto alitupwa. Picha na Ben Gadau

Aidha Limbu Mazoye ni kaimu Mganga mkuu wa Manispaa ya Mpanda ambapo mtoto huyo anapatiwa matibabu amesema kwa sasa hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika huku akiwaaasa wananchi kuacha kutenda matukio hayo ya kikatili.

Sauti ya kaimu Mganga mkuu wa Manispaa ya Mpanda akieleza kuhusu hatua za matibabu ya mtoto huyo

Kaster Ngonyani kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema kuwa tayari mhusika wa tukio hilo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi huku akiwataka wananchi kuacha kufanya matukio ya namna hiyo.

Sauti ya kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonani akizungumzia hatua iliochukuliwa kuhusu Mshakiwa wa tukio hilo.

Tukio hilo limetokea February 10 usiku katika mtaa wa mlimani site kata ya uwanja wa ndege.