Mpanda FM

Wanawake Waaswa Kuwa Wabunifu

6 September 2023, 10:18 am

MPANDA

Baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa maoni mseto juu ya namna gani wanawake wanaweza kuchangamkia fursa za uvumbuzi na ubunifu katika kujitafutia kipato na kuondokana na umaskini.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm kwa nyakati tofauti na kuongeza kuwa kikubwa wanapaswa kujiamini ili watu wengine waweze kujiamini

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Mpanda Marieta Mlozi amesema kuwa wao kama Manispaa ya Mpanda wamekua wakiwasaidia katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kupata mikopo na kuwahamasisha zaidi kujifunza ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Kwa mujibu wa utafiti wa after access wa 2018 umebaini kuwa Nchi maskini zaidi kutoka afrika kama vile Rwanda Tanzania na msumbiji zilionyesha tofauti kubwa ya kijinsia katika upatkanaji na matumizi ya teknolojia (ICT) huku wanawake wakiwa katika hali ya chini ukilinganisha na wanaume.

#mpandaradiofm97.0

#maendeleoyajamii