Mpanda FM

Baadhi ya wazazi, walezi Katavi walalamikia walimu kutoza fedha wanafunzi

10 October 2024, 5:17 pm

picha na mtandao

“Wanatozwa pesa  kiasi cha shilingi 200 kwa kila mwananafunzi kila siku”

Na Leah Kamala -Katavi

Baadhi ya wazazi  na walezi wanaosomesha watoto wao katika shule ya msingi Muungano ,manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia suala la mchango hasa kwa masomo ya muda wa ziada.

 hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya watoto kusoma masomo ya ziada katika shule hiyo huku wazazi hao wakidai kuwa wanatozwa pesa  kiasi cha shilingi 200 kwa kila mwananafunzi kila siku

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazazi hao wamewaomba walimu hao kuwa wafute masomo ya ziada na ubaki muda wa unaojulikana na serikali .

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Teresia Peter Kijika  amekanusha suala la wanafunzi kudaiwa pesa ya masomo ya ziada (TWISHENI)  Na kuongeza kuwa kazi ya ualimu ni wito hivyo wao walimu wanajitoa kwa moyo kuhakikisha watoto wanafanya vizuri katika masomo yao.

Sauti ya mwalimu mkuu akizungumzia suala hilo

Aidha mwalimu huyo amebainisha faida za kuwepo na masomo  rekebishi kwa watoto hivyo wazazi waweke nguvu katika kuwasimamia watoto wao.

Sauti ya mwalimu mkuu akizungumza

Naye peter chandalala ambae ni mwenyekiti wa shule hiyo  amesema kuwa wazazi wengi hawazungumzi na watoto wao pindi wanaporudi nyumbani hali inayopelekea wazazi kutokuelewa nini kinaendelea shuleni.

Mwenyekiti wa kamat i ya shule akieleza