Mpanda FM

Madiwani Waishauri Serikali kuhusu TASAF

26 July 2023, 6:00 pm

MPANDA

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameishauri serikali kuzipitia changamoto zilizopo katika mpango wa kunusuru kaya Maskini TASAF ikiwa ni Pamoja na malipo ili kuufanya mpango huo kuwa na manufaa kwa walengwa .

Ushauri huo wameutoa wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kufunga mwaka wa fedha 2022/2023 na kusema kuwa nia ya serikali kuanzisha mpango huo ulikuwa ni kupunguza umaskini katika jamii.

Wananchi wakizungumza juu ya mpango huo wamelalamikia uwepo wa upendeleo wakati wa mchakato wa upatikanaji wa majina ya walengwa jambo ambalo wamesema kuwa linakwamisha malengo ya serikali

Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda afisa maendeleo ya jamii Marieta Mlozi amesema kuwa hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na serikali ili kuuboresha mfumo huo.

#mpandaradiofm97.0

#tasaf