Mpanda FM

TCRA yatoa mafunzo Mpanda Radio Fm

12 June 2023, 2:40 pm

MPANDA

Vyombo vya habari mkoani Katavi vimetakiwa kufuata sheria, kanuni na miongozo pamoja na kulinda haki ya mtoto na kutokutoa vipindi vyenye maudhui yenye lugha ya matusi.

Hayo yamebainishwa na Josephine Ndeje afisa mahusiano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA] makao makuu wakati akitoa mafunzo kwa wandishi wa habari na watangazaji wa kituo cha radio cha Mpanda Fm kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi juu ya kazi hiyo.

Kwa upande wa wandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru TCRA kwa kutoa mafunzo hayo ambayo wamesema yatasaidia kuongeza utendaji bora katika kazi zao.

Miongoni mwa mambo yaliyofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na vyombo vya habari kuhakikisha vipindi vinavyorushwa vinaendana na mila na desturi za jamii.

#mpandaradiofm97.0

#katavists

#tcra