Mpanda FM

Wakulima watakiwa kutumia mizani sahihi kuuza mazao

20 May 2026, 3:05 pm

Meneja wakala wa vipimo mkoa wa Katavi Mrinde Elihaki. picha na Anna Milanzi

Na Anna Milanzi-Katavi

Wakulima  mkoani  Katavi  wameshauriwa kutumia mizani katika mauzo ya mazao  na kuachana na Vipimo batili.

Katika kuadhimisha siku ya vipimo duniani meneja wakala wa vipimo mkoa wa Katavi Mrinde Elihaki amewashauri wakulima kuzingatia matumizi ya vipimo halali na kuacha kukubaliana na vipimo visivyo rasmi

Ameyasema hayo alipokuwa katika kipindi cha kumekucha Tanzania kinachorushwa kupitia Mpanda redio FM may 20, 2026.

Sauti ya meneja wakala wa vipimo mkoa wa Katavi

Kufuati uwepo wa siku hii, wananchi  mkoani Katavi wametoa ombi kwa wakala wa vipimo mkoa wa Katavi kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi ili waweze kutambua umuhimu wa kutumia Vipimo ikiwemo mizani.

Sauti ya wananchi mkoa wa Katavi

Kaulimbiu ya mwaka huu inasema sayansi ya vipimo isaidie kujenga imani katika utungaji wa sera .