Mpanda FM

RC Katavi awapongeza na kuwatakia kila la heri wanafunzi kidato cha nne

20 November 2023, 7:35 pm

Picha na Mtandao

Jumla ya Wanafunzi 5233 wanafanya mtihani wa kuhitimu kidato cha Nne Mkoani Katavi ambapo Mkuu wa Mkoa huo amewapongeza walimu wote kwa maandalizi ya kuhakikisha wanafunzi  wanafanya vizuri

Na Betrod Benjamini -Katavi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewapongeza na kuwatakia heri wanafunzi wa kidato cha nne mkoani hapa ambao wameanza mtihani wa kuhitimu masomo yao tarehe 13 mwezi Novemba mwaka  huu.

Mrindoko amebainisha hayo mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa maandalizi walioyafanya walimu na wanafunzi yakazae matunda kwa kufanya mtihani  vizuri ili waweze kufaulu na kueleza kuwa mkoa una shule za kukidhi mahitaji kwa ajili kidato cha tano na sita.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi

Aidha Mrindoko amesema kuwa jumla ya wanafunzi 5,233 wanafanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mkoani Katavi huku akiwapongeza walimu wote kwa maandalizi ya kuhakikisha wanafunzi  wanafanya vizuri katika mtihani wao.

Picha na Betrod Benjamini

Jumla ya wanafunzi wa kidato cha nne 572,338 nchini Tanzania wameanza mtihani wao wa kuhitimu tarehe 13 ambapo wanatarajiwa kumaliza Novemba 30 Mwaka 2023.