Mpanda FM

Madawati 30,000 kunusuru wanafunzi kukaa chini Katavi

20 February 2024, 12:29 pm

Picha na Deus Daud

Mkoa wa Katavi unatarajia kutatua kero katika miundombinu ya Elimu ikiwemo ujenzi wa Maboma zaidi ya 500 ambayo kati yake 400 yako katika hatua za umaliziaji kimkoa kwa shule za Msingi na Sekondari na madawati 30,000 thelathini elfu kwa mkoa mzima.

Na Festo Kinyogoto-Katavi.

Chuo cha Ufundi stadi VETA mkoa wa Katavi kimepewa tenda ya kutengeneza Madawati 6500 katika kutatua kero ya Upungufu Madawani Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani katavi ifikapo June mwaka huu.

Akizungumza katika kata ya shanwe  mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya manisapaa ya Mpanda Bi Sophia Kumbuli amsema kuwa Manispaa ya Mpanda imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kukusanya Mbao kwaajili ya kutengeneza Madawati ambapo mpaka sasa chuo hicho kimetengeneza madawati 578 huku lengo la Manispaa ikiwa ni kutengeneza Madawati 6,000.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya manisapaa ya Mpanda Bi Sophia Kumbuli akizungumza mkakati wa manispaa kukamilisha Madawato 6000 ili kunurusu wanafunzi kukaa Chini.

Mkuu wa chuo cha Veta Mpanda Joshua Matagane amemuomba mkuu wa mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na wadau wanaohusika na uchakataji wa Mbao kufikisha kwa wakati kwakuwa mwanzo utengenezaji ulikuwa unasua sua kwa sababu ya ucheleweshwaji wa mchakato wa uletaji Mbao pamoja na changamoto ya umeme iliyokuwa inakwamisha zoezi hilo.

Sauti ya Mkuu wa chuo cha Veta Mpanda Joshua Matagane akizungumza kuhusu hatua waliofikia ya utengenezaji Madawati waliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda.

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amesema mkoa wa Katavi unatarajia kutatua kero katika miundombinu ya Elimu ikiwemo ujenzi wa Maboma zaidi ya 500 ambayo kati yake 400 yako katika hatua za umaliziaji kimkoa kwa shule za Msingi na Sekondari na madawati 30,000 thelathini elfu kwa mkoa mzima.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza mkakati wa mkoa kutatua changamoto ya miundombinu ya elimu kwa Majengo na Madawati.

Mkuu wa mkoa wa katavi alipokuwa akikabidhi madawati kwa baadhi ya shue ambayo tayari yamekamilika kwa Manspaa ya Mpanda. Picha na Deus Daud

Aidha Mwanamvua ameipongeza halmashauri ya Manisapaa ya Mpanda kwa kuwa ya kwanza kukabidhi madawati 578 ya awali hivyo halmashauri zingine zinatakiwa kuharakisha ili kufanikisha maazimio ya mkoa kutengeneza Madawati elfu 30 ,000 na Maboma 500.