Mpanda FM

Mkuu wa Mkoa Katavi Awaonya Viongozi Kuhusu Uhalifu

20 November 2021, 11:45 am

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka viongozi wa serikali kutokuwa chanzo cha kukumbatia uharifu katika jamii.

 Akizungumza na Mpanda Radio Fm amesema kumekuwa na tabia kwa  baadhi ya viongozi wa serikali kutumia nafasi zao za kazi kuwatetea waharifu pindi wanapokuwa wametiwa hatiani. 

Sauti ya Mkuu wa Mkoa

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi ACP Benjamini Kuzaga amesema ulinzi wa raia na mali zake sio jukumu la polisi peke ake bali ni wajibu wa kila mtu  huku akiwataka  baadhi ya  viongozi wa serikali za mitaa  kuacha tabia ya kuwaficha waharifu katika maeneo yao.

Sauti ya RPC

 Sambamba na hilo Kuzaga ameeleza kuwa Jeshi la polisi  limekuwa likijitahidi kudhibiti matukio ya kiharifu licha ya kutopewa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa  wananchi na viongozi wa mitaa