Mpanda FM
Mpanda FM
12 December 2025, 6:19 pm

Viongozi wa walmashauri ya Mpanda katikati ni mkuu wa wilaya Jamila Yusuph. Picha na Samwel Mbugi
“Kwa mwaka 2025/2026 halmashauri imejipanga kupokea na kukusanya jumla ya billion 7”
Na Samwel Mbugi
Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi imepanga kukusanya mapato ya Billioni 7 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akitoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za halmashauri ya manispaa ya Mpanda kupitia kikao cha kamati ya ushauri afisa mipango Leonard Kilamhama amesema mpaka kufikia November 2025 halmashauri imekusanya billion 2.1 kati ya billion 7.
Kwa upande wake Mstahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Charles Venas Philipo amesema kuwa wamejipanga kusimamia mapato ya ndani kwa baadhi ya vyazo kuviwekea CCTV kwa lengo la kudhibiti upotevu wa mapato.
Hata hivyo mkuu wa wilaya Jamila Yusuph ambae alikuwa mwenyekiti wa kikao amesema ipo haja ya kufanya ziara kwenye miradi ikihusisha viongozi wa dini na vyama vya siasa kwenda kukagua miradi hiyo.
Jamila ametoa wito kwa watumishi wa umma kuwa na lugha nzuri katika kazi zao kama maadili na miongozo unavyoelekeza.