Mpanda FM
Mpanda FM
8 August 2024, 9:51 am

picha na mtandao
“kukatika kwa umeme mara kwa mara kunasababisha kushuka kiuchumi ambapo wafanyabiashara hao wanajikuta wanakuwa na kipato duni”
Na John Benjamin- Katavi
Wafanyabiashara manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia adha ya kukatika kwa umeme mra kwa mara hali ambayo inawasababishia hasara
Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara wakati wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti na kueleza kuwa Uchumi wao unayumba kutokana na shughuli zao kuhitaji umeme.
Sauti ya wafanyabiashara wakizungumza juu ya changamoto ya umeme
Akizungumza kwa njia ya simu afisa mahusiano wa shirika la umeme Tanzania mkoa wa Katavi Proches Joseph amesema kuwa kumekuwa na maboresho kwa baadhi ya laini ya nishati hiyo ya umeme.
Sauti ya afisa mahusiano wa shirika la umeme Tanzania mkoa wa katavi Proches Joseph
Kwa mujibu wa taarifa hiyo maboresho yanayofanyika ni kwa ajili ya maandalizi ya mapokezi ya umeme wa gridi ya taifa mwezi ujao