Mpanda FM

Acheni kuishi na kuku, fugeni kuku

7 July 2025, 7:34 pm

Wajasiriamali wakiwa kwenye mafunzo. Picha na Anna Mhina

“Lengo ni kuhakikisha wanakatavi wanapata mafunzo ya uchumi na ujasiriamali”

Na Anna Mhina

Zaidi ya wajasiriamali 80 mkoani Katavi wamepatiwa mafunzo ya namana ya ufugaji bora wa kuku, utengenezaji wa sabuni pamoja na utengenezaji wa batiki.

Akizungumza na Mpanda radio FM mwalimu  Benjamin Chahe kutoka chuo cha Mkwawa V.T.C kilichopo Iringa ameeleza lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwakwamua kiuchumi wananchi wa katavi.

Sauti ya mwalimu Benjamini

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza namna walivyonufaika na mafunzo hayo na kuahidi kuyatendea kazi ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya washiriki

Mafunzo hayo yameandaliwa na Mpanda radio FM kwa kushirikiana na chuo cha Mkwawa VTC kilichopo Iringa mjini ambapo yatafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa CCM wilaya ya Mpanda.