Mpanda FM

Katavi: Ombi la rufaa lakubaliwa kutofukuliwa mwili wa Bukuku

29 April 2024, 7:05 pm

Kaburi la marehemu Lwitiko Bukuku. Picha na Anna Milanzi

Wazazi wa marehemu Lwitiko hawatambua kama mtoto wao huyo aliwahi kubadili dini na kuwa mwislam

Na Samwel Mbugi-Katavi

Familia ya marehemu aliyefahamika kwa jina la Lwitiko Bukuku imeiomba mahakama kutenda haki katika kesi  iliyofunguliwa na anayejieleza kuwa ni mke wa marehemu akidai mumewe amezikwa kwa imani ya dini ya Kikristo badala ya imani ya Kiislamu.

Hayo yamesemwa na dada na kaka wa marehemu Mary Bukuku na Edward Bukuku wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm kuwa kesi hiyo imeleta taharuki kwa ndugu na jamaa kwani wao kama familia hawakujua kama marehemu alikuwa amebadili dini.

Sauti za dada na kaka wa marehemu Mary Bukuku na Edward Bukuku
Edward Bukuku kaka wa Marehemu picha na Anna Milanzi
Merry Bukuku dada wa marehemu. Picha na Anna Milanzi

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi mmoja Mussa Alfani amesema kuwa tarifa za ufukuaji wa kabuli ni za kweli na zilileta taharuki  kwa wanachi wa mtaa huo kwani tukio hilo ni mara ya kwanza kutokea katika mtaa wake.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnazimmoja akizungumza
Musa Alfani mwenyekiti Mtaa wa Mnazi mmoja. Picha na Anna Milanzi

Pia Mussa amewataka wananchi wanaomzushia kuwa ameegemea upande mmoja waache mara moja kwani yeye anasimamia haki ya kila mwananchi wa mtaa wake tofauti na wanavyofikilia kuwa yuko upande wa familia ya marehemu.

Sauti ya Mwenyekiti Mtaa wa Mnazimmoja
Picha ya marehemu Lwitiko Bukuku enzi za uhai wake

Hata hivyo Mahakama ya wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi imekubali ombi la rufaa kwa ndugu wa marehemu ambayo imesikilizwa Aprili 29, 2024 ya zuio la kufukua mwili wa marehemu ambapo ulipaswa kufukuliwa na kuzikwa upya kwa imani ya dini ya Kiisilam ,na kesi hiyo itapangwa tarehe ya kusikiliza tena.