Mpanda FM

Mpanda-Wananchi msitelekeze wagonjwa hospitali

9 February 2024, 3:08 pm

Baadhi ya wagonjwa wanaofikishwa katika hospital Hutelekezwa na ndugu zao    na kuleta mzigo kwa serikali.Picha na Mtandao

Na Veronica Mabwile-Katavi.

Wito umetolewa kwa wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi   kuacha taabia  ya    kuwatelekeza   wagonjwa wakati wakupatiwa  huduma za matibabu ili kuipunguzia mzigo.

Wito huo  umetolewa na Mganga mfawidhi hospital ya Manispaa ya  mpanda DK   PAUL LUGATA wakati akiongea na kituo  hiki na kusema kuwa wapo  baadhi ya wagonjwa wanaofikishwa katika hospital hiyo na kutelekezwa na ndugu zao    na kuleta mzigo kwa serikali.

Sauti ya Mganga mfawidhi hospital ya Manispaa ya  mpanda DK   PAUL LUGATA.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa  chanzo cha  wagonjwa kutelekezwa wakati wa kupatiwa na matibabu inatokana na hali  duni ya uchumi kumudu gharama za matibabu sambamba na kupungua kwa hali ya kujali kwa baadhi ya wanajamii. 

Sauti ya wananchi wakieleza kuhusu sababu za kutelekeza wagonjwa hospitali

Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii katika hospital hiyo ANIRUMI LONGO amesema kuwa niwajibu wa jamii kushirikiana na serikali ili kuwasaidia Wwagonjwa ambao wanapitia changamoto za kiuchumi wakati wa matibabu.

Sauti ya afisa ustawi wa jamii katika hospital hiyo ANIRUMI LONGO.

Kumekuwepo kwa changamoto ya baadhi wagonjwa kutelekezwa  katika vituo vya  afya na hospitali  jambo ambalo limekuwa likiibua mkanganyiko kwa watoa huduma .