Mpanda FM

Wananchi Kasekese waishukuru serikali kwa kuwajengea shule mpya

5 October 2023, 2:01 pm

Onesmo Buswelu na baadhi ya wananchi mara baada ya ukaguzi wa shule

Wananchi wa kijiji cha Magogo kata Kasekese wilaya ya Tanganyika mkoani  Katavi wameishukuru serikali kwa kuwajengea shule kijijini hapo.

Na Gladness Richard – Tanganyika

Wananchi wa kijiji cha Magogo kata Kasekese wilaya ya Tanganyika mkoani  hapa wameishukuru serikali kwa kuwajengea shule mpya kijijini hapo.

Wakizungumza na Mpanda radio Fm wananchi hao wamesema kuwa watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu na hali hiyo iliwafanya wawe na hofu juu ya usalama wa watoto.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake mkurugenzi wa wilaya ya Tanganyika Shaban Juma amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo mpya utapunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Kasekese.

Sauti ya Mkurugenzi

Ujenzi huo umeambatana na madarasa sita mapya, vyoo na nyumba moja ya mtumishi huku chanzo cha fedha hiyo kikiwa ni serikali kuu.