Mpanda FM

Watoto waangukiwa na ukuta Katavi, mmoja afariki

12 April 2024, 8:55 pm

Nyumba ambayo ukuta wake umeanguka na kuwaangukia Watoto Wawili ambapo Mmoja kati yao amefariki .Picha na Deus Daud

Baada ya Mvua Kunyesha na Maji kuwa mengi  yamezunguka  Nyumba na kusababisha kuanguka kwa Ukuta wa Nyumba hiyo

Na Lilian Vicent -Katavi

Mtoto Mmoja Mwenye Umri wa  Miaka Mitano amepoteza Maisha  na Mwingine amepata Majeraha baada ya kuangukiwa na Ukuta wa Nyumba waliyokuwa wakiishi  kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha   Mkoani hapa.

Wakizungumza na Mpanda Redio Fm  Mashuhuda Wa  tukio hilo lililotokea  Mtaa Kapalangao Kata ya        Kazima Mkoani Katavi wamesema    baada ya Mvua kunyesha na Maji kuwa Mengi  yamezunguka  Nyumba na kusababisha kuanguka kwa Ukuta wa Nyumba hiyo.

Sauti za Mashuhuda Wa  tukio hilo lililotokea  Mtaa Kapalangao Kata ya    Kazima

Kwa  upande wake Mama Mzazi wa Watoto hao Zainabu Hamimu   ameeleza kuwa Watoto wake walikuwa wamelala wakati Mvua ikinyesha kabla ya tukio hilo kutokea .

Sauti ya Mama Mzazi wa Watoto Walioangukiwa na Ukuta akieleza Tukio lilivyokuwa

Nae Diwani wa kata ya  Kazima Linus Evarist  amesema alipokea Taarifa ya tukio hilo na baadae alifika eneo la  tukio kwenda kushuhudia  na ameongeza kuwa  Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimechangia kwa kiasi kikubwa Ukuta wa Nyumba hiyo Kuanguka .

Sauti ya Diwani wa kata ya  Kazima Linus Evarist akilielezea Tukio hilo

Akithibitisha kutokea kwa  tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani  hapa Kaster Ngonyani ametoa wito kwa Wakazi wa Maeneo hayo kuchukua Tahadhari hususani katika  kipindi  hiki cha Mvua.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akithibitisha tukio hilo

Ikumbukwe kuwa Tukio hilo limetokea usiku wa  April 8 Mwaka huu Mtaa wa Kapalangao kata ya Kazima mkoani Katavi kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa na kuleta athari katika baadhi ya Maeneo.Ili kuitazama Video ya taarifa hii bonyeza hapa