Mpanda FM

Katavi: Wawili jela miaka mitatu mauaji bila kukusudia

7 June 2023, 5:36 pm

KATAVI

Watu wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kila mmoja mara baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia mkoani Katavi huku watu wengine wanne wakienda jela kwa makosa ya wizi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi wa Polisi Ali Makame Hamad ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema hukumu za kesi hizo ni miongoni mwa mafanikio ya kesi mbalimbali zilizofikishwa mahakamani na jeshi la polisi.

Mbali ya watuhumiwa hao, watu wengine wanne wamehukumiwa vifungo mbalimbali na faini kwa makosa mbalimbali ya wizi.

Akizungumzia hali ya usalama katika mkoa wa Katavi alipoulizwa na wanahabari juu ya suala la makundi ya damu chafu, Kamanda Ali Makame Hamad ameeleza hatua zilizochukuliwa dhidi yao .

Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wote mkoani Katavi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kutoa taarifa zote zenye viashiria vya uhalifu kwa wakati kwa kuwatumia wakaguzi kata waliopo kwenye maeneo yote mkoani Katavi.

#mpandaradiofm97.0

#katavists

#wizarayatamisemi