Mpanda FM

Madiwani Tanganyika watakiwa kusimamia miradi inayoanzishwa na wananchi

14 September 2023, 12:18 pm

Picha na Mtandao

Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya serikali na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.

Na Kilian Samwel – Tanganyika
Madiwani halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi wametakiwa kusimamia miradi inayoanzishwa na wananchi pamoja na kuwashirikisha katika miradi mbalimbali ya serikali.

kufikia tarehe 15 mwezi huu kutoa taarifa ya hatua gani ilipofikia miradi yote ndani ya halmashauri ambayo haijakamilika.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso wakati wa baraza la madiwani halmashauri ya Tanganyika ambapo amesema madiwani wanawajibu wa kuwashirikisha wananchi kwenye miradi ya serikali.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Selemani Kakoso

Mwenyekiti wa halmashauri ya Tanganyika Hamad Mapengo amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika kufikia tarehe 15 mwezi huu kutoa taarifa ya hatua gani ilipofikia miradi yote ndani ya halmashauri ambayo haijakamilika.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tanganyioka Hamad Mapengo

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dr. Alex Mrema amesema serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya serikali na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika Alex Mrema