Mpanda FM

TARURA Mpanda kuboresha barabara

30 June 2023, 10:31 am

MPANDA.

Meneja wa Tarura wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Kahose Joseph ameeleza namna Tarura inavyotenda kazi katika barabara zilizo chini ya mamlaka hiyo.

Kahose Joseph amebainisha hayo wakati akizungumza na Mpanda redio fm amesema lengo ni kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya Barabara ambazo zinapaswa kuboreshwa chini ya mamlaka hiyo.

Aidha Kahose ameendelea kuzungumza kwa kutolea ufafanuzi kuhusu uboreshaji wa Barabara ya kijiji cha Ivungwe kata ya kasokola Manispaa ya Mpanda ambapo amesema tayari wamekwisha kuandika barua kwa Waziri mwenye dhamana ili Barabara hiyo iendelee kuhudumiwa chini yao.

Hivi karibuni wananchi wa Kijiji cha ivungwe wamenukuliwa wakilalamikia changamoto ya miundombinu ya Barabara ambapo wamesema kuwa mara ya mwisho Barabara hiyo kufanyiwa marekebisho ilikuwa mwaka 2009.

#mpandaradiofm97.0

#tarura

#tanroad