Mpanda FM

Watatu wauwawa kikatili Katavi

6 May 2024, 5:29 pm

Ndugu hao wameiomba serikali kuhakikisha inatenda haki katika tukio hilo ambalo ni La kikatili na lakusikitisha kwani ni mara yakwanza kutokea katika familia yao” Picha na mtandao

Na Samwel Mbugi-Katavi

Watu watatu wa familia moja wameuawa kikatili na mtu/watu wasiojulikana katika Kijiji cha Bulamata Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi.

Hayo yamethibitishwa na Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Dkt Mundhiri Bashiri akizungumza na Mpanda Radio Fm kuwa ni kweli wamepokea miili ya watu watatu wa familia moja Mama na Watoto wake wawili,  ambao ni Monica Shire (24), Siwema Shija (02) na Yanga Shija mwenye umri wa miezi Nane.

Sauti ya Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Dkt Mundhiri Bashiri akizungumza jinsi walivyopokea miili hiyo.

Picha ya Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Dkt Mundhiri Bashiri akizungumza jinsi walivyopokea miili hiyo.Picha na Anna Milanzi

Kwa upande wao ndugu wa marehem wamesema kuwa walipokea tarifa hizo kutoka kwa mdogo wao akiwaeleza kuwa amekuta familia yake imekatwa mapanga na Mtu /Watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Sauti ya Ndugu wa marehem akieleza jinsi walivyopokea taarifa hizo.

Pia ndugu hao wameiomba serikali kuhakikisha inatenda haki katika tukio hilo ambalo ni La kikatili na lakusikitisha kwani ni mara yakwanza kutokea katika familia yao.

Sauti ya Ndugu wa marehem akiomba hatua zaidi zichukuliwe kwa waliofanya mauaji hayo pale watakapobainika.

Ndugu wa mume wa marehem Jumanne Shija na Kulwa Shija wakiwa katika hospiali ya manispaa wakisubiri kuchukua miili ya marehemu kwa ajili ya mazishi Picha na Anna Mila

Hata hivyo juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Caster Ngonyani zimefanyika na kusema kuwa upelelezi unaendelea kuhusiana na tukio hilo ambalo limetokea wilaya ya Tanganyika mkoa wa katavi na taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni.