Mpanda FM

Kati ya watu 100 Katavi, mmoja kati yao ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi

4 December 2023, 11:06 am

Picha na Mtandao

Asilimia 5.4% ya wananchi mkoani Katavi wana maambukizi  ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Na Gladness Richard-Katavi

Imeelezwa kuwa Kati ya Watu 100 Mmoja kati yao ana Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Mkoani Katavi.

Takwimu hizo Zimetolewa na Daktari kutoka katika Hospitali ya Mkoa wa Katavi Kitengo cha Matibabu, Upimaji wa hiari wa Virusi Vya Ukimwi Salvius Ngahyolerwa ambapo amesema Asilimia 5.4% ya Wananchi Mkoani Katavi wana Maambukizi  ya Virusi Vya Ukimwi.

Sauti ya Daktari kutoka katika Hospitali ya Mkoa wa Katavi Kitengo cha Matibabu, Upimaji wa hiari wa Virusi Vya Ukimwi

Kwa upande wao baadhi ya Wagonjwa ambao Wanaishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi wamesema kuwa kwa mara ya kwanza walipogundua wana Ugonjwa huo walifadhaika lakini kwa sasa wamekubaliana na hali hiyo na kuwashauri wengine walioathirika kukubali na kutumia dawa za kufubaza Maambukizi ya Ugonjwa huo.

Sauti ya Wagonjwa ambao Wanaishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi

Hata hivyo Wananchi nao Wamesema kuwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi anaishi nao Vizuri huku Wakiwashauri Waendelee Kutumia dawa.

Sauti za Wananchi Wakizungumza kutowanyanyapaa Wagonjwa Wenye Virusi vya Ukimwi

Siku ya Ukimwi dunia huazimishwa kila ifikapo December Mosi kila Mwaka na Mwaka huu imeambatana na kauli mbiu isemayo “Jamii iongeze kutokomeza Ukimwi”.