Mpanda FM

Waandishi wa habari nyanda za juu kusini wanufaika na mafunzo ya Tadio

12 September 2023, 7:27 am

Baadhi ya waandishi wakiwa katika makundi wakijadiliana kuhusu mafunzo. Picha na Lusy Dashud

Mafunzo haya yatawasaidia waandishi wa habari kuwa na uelewa zaidi kidigital kwa kuchapisha Habari ,Makala  na kufikisha elimu mbalimmbali kupitia radio tadio

Na Anna Millanzi – Mbeya

Waandishi wa Habari wa radio jamii nyanda za juu kusini wamepatiwa mafunzo ili kufanya kazi zao kwa weledi na kutumia fursa Iliyopo kwa kuendana na teknolojia.

lengo la mafunzo hayo ni kuwafundisha namna ya kuandaa na kusambaza habari zao kupitia teknolojia kwa njia ya mtandao na kuwainua kichumi kwa kutumia mitandao.

Mafunzo hayo yamewakutanisha  Wahariri Pamoja na Waandishi wa habari kutoka vituo vya radio tisa ukanda wa  Nyanda za juu kusini ili kuwajengea uwezo .

Akizungumza mara baada ya kutolewa mafunzo hayo Afisa  miradi Saumu Bakari wa mtandao wa radio jamii Tanzania (TADIO)amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafundisha namna ya kuandaa na kusambaza habari zao kupitia teknolojia kwa njia ya mtandao na kuwainua kichumi kwa kutumia mitandao.

Sauti ya Saumu Bakari Afisa Miradi wa Tadio

Mwezeshaji Wa mafunzo hayo  Amua Rushita ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kuwa na uelewa zaidi kidigital kwa kuchapisha Habari,Makala  na kufikisha elimu mbalimmbali kupitia radio tadio.

Sauti ya Amua Rushita Mwezeshaji wa Mafunzo Tadio

Baadhi ya waandishi wa habari katika mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yanatija kwao kwani yanakwenda kubadilisha mitazamo na kuongeza fursa kuifikia jamii na kuongeza uchumi wa radio.

Sauti ya Baadhi ya Waandishi Walionufaika na mafunzo hayo