Mpanda FM
Mpanda FM
10 September 2026, 10:07 am

“mashamba yangu yote yalikumbwa na mtaro wa maji”
Na. Restuta Nyondo
Wakulima katika Kijiji cha Mnyagala wamelishukuru shirika la SNV kwa kusaidia kurejesha mto katika njia yake na kuokoa mashamba yao ambayo yamekua yakipotea kila mwaka.
Wameiambia mpanda radio fm kuwa baadhi wamekuwa wakipoteza zaidi ya ekari 100 na kupoteza uzalishaji wa mazao kusombwa na maji baada ya mto huo kupoteza njia yake ya asili na kuwasababishia hali mbaya kiuchumi.
Bruno Richard ni meneja mradi wa IKI KATUMA anayefanya kazi na SNV amesema kuwa mto huo ulihama njia kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kuchepusha maji hali iliyoathiri wakulima kwa kusababisha mafuriko kutokana na asilimia 60 ya maji yalikua yanaenda kwenye mashamba.
Aidha Mhandisi Almasi Mlala kutoka katika bonde la maji la ziwa Rukwa amesema kuwa shughuli hiyo ya urejeshwaji wa mto katika njia yake ya asili kuna gharimu kiasi kikubwa cha fedha na kuwataka wakulima kuacha tabia ya kuchepusha maji na kuwa walinzi wa mto huo na vyanzo vyote vya maji.