Mpanda FM

Mpanda yaanza kuchukua tahadhari El-Nino

7 September 2026, 2:56 pm

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Kimaro. Picha na Saga

Na. Ben Gadau

Wananchi wasibeze taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamil Yusuph Kimaro, amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El-Nino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza katika kipindi cha Kumekucha Tanzania, DC Jamila amewataka wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni na maeneo hatarishi kuchukua hatua mapema, ikiwemo kuhama maeneo hayo na kwenda sehemu salama, ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mafuriko na kujaa kwa maji.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

Aidha, Jamila amewataka wananchi kuwa makini katika maeneo ya migodi, mito na maeneo mengine hatarishi, huku akisisitiza umuhimu wa kusafisha mifereji ya maji na kuzingatia taarifa na maelekezo yanayotolewa na mamlaka.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

DC Jamila amesema maandalizi ya mapema ni muhimu katika kulinda maisha, mali na shughuli za wananchi wakati wa msimu huo wa mvua.