Mpanda FM
Mpanda FM
4 September 2026, 12:34 pm

Na Ben Gadau
Mkoa wa Katavi unatarajia kuzindua Kamati za Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya, Septemba 8, 2026 kwenye Viwanja vya Azimio mjini Mpanda, ambapo wananchi wa Katavi na mikoa jirani watapata huduma za Kliniki ya sheria bila Malipo.
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 3, 2026, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Albert Msovela, amesema kliniki hiyo itafanyika kuanzia Septemba 7 hadi 13, 2026, katika Viwanja vya Azimio, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.
Amesema wananchi watapata fursa ya kupata ufafanuzi kuhusu haki zao, wajibu wao pamoja na hatua na taratibu sahihi za kufuata katika kushughulikia changamoto mbalimbali za kisheria.
Bw. Msovela amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kupata elimu na ushauri wa kisheria bila malipo, ili kuongeza uelewa kuhusu haki zao na namna sahihi ya kutatua changamoto za kisheria.