Mpanda FM
Mpanda FM
7 October 2026, 5:09 pm

“huu sio utamaduni wetu watu waache imani za kishirikina“
Na Samweli Mbugi
Kaburi la mtoto mwenye umri wa miezi mitatu, aliyefariki dunia na kuzikwa mwezi mmoja uliopita katika Makaburi ya Mwangaza, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, limefukuliwa na watu wasiojulikana, huku tukio hilo likihusishwa na imani za kishirikina.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mama wa mtoto huyo amesema alikuwa mtu wa kwanza kushuhudia kaburi la mwanawe limefukuliwa alipokuwa akipita katika makaburi hayo kuelekea sokoni.
Baadhi ya wananchi wakidai kulipokea kwa masikitiko tukio hilo na kuiomba Serikali pamoja na vyombo vya usalama kuongeza ulinzi katika eneo hilo ili kuwabaini watu wanaohusika na matukio kama hayo.
Kwa upande wao, Wenyeviti wa Mitaa ya Mpadeko na Mwangaza wamesema walipokea taarifa kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo, na baada ya kufika eneo la tukio walijionea hali hiyo, huku wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Baada ya uchunguzi kufanyika, ilibainika kuwa watu hao walishindwa kuutoa mwili uliokuwa ndani ya kaburi, licha ya kufukua makaburi mawili ya watoto waliozikwa katika eneo hilo