Mpanda FM
Mpanda FM
6 November 2026, 10:59 am

“tumeleta hapa Mwamkulu kwasababu kuna skimu kubwa ya umwagiliaji“
Na. Betord Chove
Jumla ya wanawake na vijana 215 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya miezi miwili ya jenga kesho iliyo bora BBT katika kata ya Mwamkulu manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Gwalusajo Kapande amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafikia vijana na wanawake ili waweze kujikita katika kilimo ili kuboresha uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Mgeni rasmi Akizungumza katika halfa ya ufunguzi wa mafunzo hayo katibu tawala wa wilaya ya Mpanda Juma Njelu kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila yusuph Ameielekeza idara ya kilimo mifugo na uvuvi kuandaa utaratibu wa kutoa ushauri ili kilimo wanachofanya kiweze kuleta tija.
Kwa upande wao wakulima washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru kwa fursa hiyo ambayo itawasaidia kuongeza uzalishaji katika kilimo chao na kuomba serikali kuendelea kuleta vitendea kazi katika sekta ya kilimo.
Mradi wa BBT { Jenga Kesho Iliyo Bora} ni programu ya kitaifa ya Serikali ya Tanzania inayolenga kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi kupitia sekta za kilimo, mifugo, na uvuvi kibiashara na Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa wizara mbalimbali (ikiwemo Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi) kwa ufadhili wa Serikali na wadau.