Mpanda FM

Kulinda mahusiano ya familia chanzo kufichwa vitendo vya ukatili

12 November 2026, 7:56 pm

Afisa ustawi wa jamii manispaa ya mpanda Anyulumye Longo akiwa ofisini kwake. Picha na Leah Kamala

“Acheni kumalizana kifamilia kesi za ukatili ili kutokomeza vitendo hivyo“

Na. Leah Kamala

Wananchi mkoani Katavi wameeleza kuwa huwa wanatoa taarifa wanaposhuhudia vitendo vya ukatili kwani vinaathiri maisha ya watu hasa wanawake na watoto.

Wakizungumza na Mpanda radio fm, kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa wapo wanaosita kuripoti kutokana na hofu na kutaka kulinda mahusiano ya kifamilia.

Sauti ya wananchi

Nae afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda Anyulumye Longo amezungumzia  sababu zinazopelekea kutokea kwa vitendo vya ukatili ikiwemo migogoro ya kifamilia na imani potofu.

Sauti ya afisa ustawi 1

Aidha Longo ameeleza athari za ukatili kuwa zinaweza kusababisha madhara ya kimwili na kuvuruga mahusiano ya kifamilia hivyo ni muhimu jamii kupatiwa elimu ili kupunguza vitendo hivyo.

Sauti ya afisa ustawi 2

Kwa upande wake afisa kutoka dawati la jinsia na watoto mkoa wa katavi Hubiri Chaula ameeleza hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na kuwataka wananchi kutoa taarifa ili kujenga jamii yenye amani.

Sauti ya askari wa dawati la jinsia na watoto