Mpanda FM
Mpanda FM
2 October 2026, 9:35 am

“acheni kuharibu vyanzo vya maji mnahatarisha afya za binadamu na viumbe hai”
Na. Bertod Chove
Wachimbaji wa madini katika bonde la Mto Katuma wametakiwa kuepuka matumizi ya kemikali ya zebaki Ili kutunza chanzo cha maji Mto Katuma.
Akizungumza katika warsha ya uwasilishaji na uthibitishaji wa matokeo ya tathmini ya athari za uchimbaji holela na uhamasishaji wa mbinu mbadala afisa maendeleo kutoka bodi ya maji bonde la ziwa Rukwa amesema ni wakati wa wataalamu kubuni mbinu mpya kuliko kuendelea matumizi ya kemikali ya zebaki ambazo sio rafiki kwenye vyanzo vya maji.
Kwa upande wao baadhi ya wachimbaji wa madini katika mto huo Katuma pamoja na mwenyekiti Martin Lutuga wakizungumza na Mpanda radio fm kuhusu uhifadhi wa mtu huo wamesema hapo awali kulikuwa na ukosefu wa mwamko wa uhifadhi pamoja na elimu hivyo elimu hiyo waliyoipata wataitumia kwenda kuwaelimisha wananchi pamoja na wachimbaji ili kuongeza uhifadhi wa bonde hilo.
Kwa upande wake Bruno Richard ambaye ni meneja wa Mradi wa IKI Katuma amesema lengo la warsha hiyo ni kuwakutanisha wataalamu na wachimbaji wadogo ili waweze kutumia mbinu mpya ambazo ni rafiki katika vyanzo vya maji.
Elimu hiyo imetolewa na bodi ya maji la ziwa rukwa kwa kushirikiana na SNV Nerthelands development organization kupitia mradi wa IKI-Katuma.