Mpanda FM
Mpanda FM
12 October 2026, 1:17 pm

“Kumekua na ongezeko la wanawake kuzungumzia ukatili wa kijinsia kutokana na ushiriki katika vikao vya maamuzi“
Na Ben Gadau
Ushiriki wa wanawake katika vikao vya maamuzi umetajwa kuwa chanzo cha mafanikio ya kupaza sauti juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia wanaopitia katika jamii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi na Atupele Myombe kwa niaba ya wanawake wameainisha kuwa wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali ikiwemo kutosikilizwa kwa changamoto zao na kuainisha kuwa elimu ambayo imekua ikitolewa imeongeza mwamko wa mwanamke kushiriki katika vikao na kuzungumzia ukatili ambao anapitia katika jamii.
Kwa upande wake George Kasambwe kutoka asasi ya TOSIVIC ameainisha baadhi ya sababu ambazo zimenyanyua mwamko wa wanawake kushiriki katika vikao vya maamuzi ili kuweza kuzungumzia ukatili wanaopitia.