Mpanda FM
Mpanda FM
10 November 2026, 7:11 pm

“tulidhani wanyamapori wangeishia tu hifadhini lakini wanafika mpaka mjini watu wa hifadhi waliangalie hili“
Na. Betord Chove
Mtoto Williams Sadik, mwenye umri wa miaka minne, ameshambuliwa na fisi katika eneo la Kilimahewa, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, tukio lililoibua hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo kutokana na wanyamapori hao kufika karibu na makazi ya watu.
Mama wa mtoto huyo pamoja akizungumza na waandishi wa habari ameeleza jinsi tukio hilo lilivotokea wakiwa katika jitihada za kutafuta usafiri kuelekea shambani.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Paul Swankala amesema hali ya mtoto inaendelea vizuri baada ya kufikishwa hospitalini hapo kwa matibabu
Kufuatia tukio hilo, wananchi wameziomba mamlaka zinazohusika na usimamizi wa wanyamapori kuongeza doria na kuimarisha ulinzi katika maeneo ya makazi ili kudhibiti wanyama hao na kuzuia mashambulizi kama hayo kujirudia.