Mpanda FM
Mpanda FM
25 November 2026, 4:30 pm

“mazingira yao sio salama tunahofia kupata magonjwa ya mlipuko “
Na. Leah Kamala
Wananchi mkoani Katavi wameeleza kuwa bado kuna changamoto ya usafi katika uandaaji na uuzaji wa chakula kwa baadhi ya migahawa hali inayoweza kuhatarisha afya za walaji.
Wakizungumza na mpanda radio fm kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema kuwa kuna baadhi ya wauzaji wa chakula ambao hawazingatii kanuni za usafi, ikiwemo usafi wa vyombo na mazingira ya kupikia chakula.
Kwa upande wao baadhi ya mama lishe na baba lishe manispaa ya Mpanda wameeleza namna wanavyotekeleza taratibu za usafi na kuahidi kuboresha huduma zao ili kulinda afya za wateja hao.
Akizungumiza suala hilo, Mratibu wa elimu ya afya kwa umma Elizabeth Sylvester ameelezea kuwa chakula kisipohifadhiwa vizuri kinaweza kusababisha vimelea vinavyotokana na magonjwa.
Aidha Elizabeth amezungumzia hatua zinazochukuliwa na mamlaka katika kutoa elimu kwa wauzaji wa chakula kufanya ukaguzi wa migahawa ili kuhakikisha wananchi wanapata chakula salama.