Mpanda FM

Kushuka wa bei ya mazao chanzo wakulima kupunguza uzalishaji mazao ya kibiashara Katavi

4 November 2026, 12:24 pm

Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Katavi Iddy Kimanta. Picha na Ben Gadau

“tusiache kuzalisha mazao ya kibiashara licha ya bei za sokoni kukatisha tamaa“

Na. Betord Chove

Wakulima mkoani Katavi wametakiwa kuendelea na shughuli za kilimo licha ya kushuka kwa bei za baadhi za mazao, ikiwamo pamba, ufuta, mbaazi na tumbaku, hali iliyosababisha baadhi yao kushindwa kurejesha madeni ya pembejeo na kuathirika kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Iddy Kimanta wakati alipotembelea mabanda ya kilimo katika maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi.

Amesema changamoto za bei za mazao hazipaswi kuwakatisha tamaa wakulima na kuwasisitiza kuendelea kuzalisha kwa kuzingatia elimu na mbinu bora za kilimo ili kuongeza mavuno na ubora wa mazao.

Sauti ya mwenyekiti Ccm

Kwa upande wake, Ofisa Kilimo Mkoa wa Katavi, Faridu Abdalah, amesema maonesho hayo yamewezesha kuwafikia wakulima wengi kwa kuwapatia elimu ya kilimo bora, huku lengo likiwa kuongeza uzalishaji na kuimarisha sekta ya kilimo mkoani humo

Sauti ya afisa kilimo