Mpanda FM
Mpanda FM
12 November 2026, 7:49 am

“tunahofia kua mitaji yetu maana hakuna kabisa wateja“
Na. Leah Kamala
Wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanya biashara zao katika soko la zamani la Kwalakwacha lililopo kata ya Nsemulwa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamegoma kuondoka katika soko hilo baada ya kutakiwa kuhamia soko jipya.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamesema miongoni mwa sababu zinazopelekea kugoma kuondoka katika eneo hilo ni kukosekana kwa wateja katika soko jipya hali inayopelekea kupoteza mitaji yao huku wengine wakidai kuwa walipewa ruhusa ya kufanya biashara na waziri mkuu.
Akijibu malalamiko hayo diwani wa kata ya Nsemulwa Alex Ngereza amekanusha hoja zao na kusema kuwa waziri mkuu alitoa maelekezo ya kurekebisha miundombinu ya soko jipya ili yatakapokamilika waende eneo husika.
Hata hivyo Ngereza amewasisitiza wafanyabiashara kuhamia soko jipya kwa lengo la kulinda afya zao na kuzuia uwezekano wa magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosekana kwa vyoo katika soko la zamani.