Mpanda FM

CCM Zanzibar kushirikana na Katavi kubadilishana fursa za kiuchumi

4 November 2026, 12:47 pm

Naibu katibu mkuu CCM Zanzibar Abdi Mahmoud. Picha na Ben Gadau

“chama kiwe na utaratibu wa kufanya ziara hadi ngazi za mitaa ili kuleta mabadiliko“

Na. Ben Gadau

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi kimefanya mkutano na wanachama wa chama hicho katika Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi, kwa lengo la kumtambulisha Mlezi wa CCM Mkoa wa Katavi, Abdi Mahamoud Abdi, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.

Akizungumza katika mkutano huo, Abdi amesema moja ya vipaumbele vyake ni kuimarisha ushirikiano kati ya mikoa ya Katavi na Zanzibar ili kuwezesha kubadilishana uzoefu, maarifa na kujifunza fursa mbalimbali za maendeleo zinazoweza kunufaisha wananchi wa pande zote mbili akisema ushirikiano huo ni muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya chama
 

Sauti ya naibu katibu mkuu

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amewataka wakulima kutumia vyema mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuimarisha shughuli za kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao, akisisitiza kuwa mvua hizo ni fursa muhimu kwa maendeleo ya sekta ya kilimo.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za chama hicho wilayani Mlele, ambapo amesisitiza dhamira yake ya kutekeleza majukumu ya ulezi kwa kushirikiana na viongozi pamoja na wanachama katika kuimarisha chama na kuendeleza maendeleo ya mkoa.