Mpanda FM

Recent posts

23 May 2022, 2:27 pm

MPANDA Vijana Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kujishughulisha na kilimo kwa kujiunga na vikundi ili kulima kilimo chenye tija zaidi. Hayo yamesemwa na wakulima wa kikundi cha AMAKWAWO wanaojishughulisha na kilimo cha zao la nyanya Wilayani Mpanda na kusema kuwa …

23 May 2022, 2:20 pm

MAZIWA NA UTOKOMEZAJI WA UDUMAVU KATAVI

Wazazi na walezi mkoani katavi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya  siku ya  maziwa  yatakayofanyika kuanzia tarehe 27 had tarehe moja mwezi wa sita mwaka  huu ili kujifunza umuhim wa  maziwa katika mwili wa mwanaadam na hatimae kuondokana na…

23 May 2022, 2:12 pm

MAADHIMISHO YA SIKU YA NYUKI KATAVI

KATAVI Kufatia maadhimisho ya siku ya nyuki duniani mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka watanzania kutunza mazingira kwa kuhifadhi misitu ili kuongeza thamani ya mazao ya mdudu nyuki. Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya nyuki duniani…

23 May 2022, 1:56 pm

MIGOGORO WAKULIMA NA WAFUGAJI HALI TETE

KATAVI. Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Karema  mkoani katavi wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kutatua mgogoro   kati ya wakulima na wafugaji kabla haujaleta madhara makubwa katika  jamii. Wakulima hao wameiambia mpanda radio fm kuwa ugomvi kati ya wafugaji…

23 May 2022, 1:42 pm

UMASKINI, CHANZO MIMBA ZA UTOTONI

KATAVI Umaskini wa kipato umetajwa Kuwa  chanzo moja wapo  cha kinachopelekea mimba  za utotoni  kwa baadhi ya familia mkoani katavi. Wakizungumza na mpanda redio fm baadhi ya wazazi hao  wameeleza namna umaskini wa familia unavyosababisha mabinti wengi kupata mimba kabla…

23 May 2022, 1:32 pm

MGANGA WA KIENYEJI MBARONI KWA ULAWITI

  Jeshi la polisi mkoani katavi limefanikiwa kumkamata mganga wa kienyeji akili abakuki almaarufu kama jimmy mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa majengo kwa tuhuma za kulawiti watoto wenye umri kati ya miaka 6 hadi 12 alipokuwa akiwapatia matibabu…

23 May 2022, 1:03 pm

DC TANGANYIKA UMEME KAREMA KABLA YA MAY 20

KATAVI. Mkuu wa wilaya ya tanganyika onesmo buswelu amelitaka shirika la umeme mkoa wa katavi kuunganisha umeme katika bandari ya karema kabla ya may 20 mwaka huu kwakuwa mradi huo upo katika hatua za mwisho kukamilika. Buswelu ametoa angizo hilo…

30 March 2022, 4:59 pm

Uvamizi Misitu: Kilio kwa Sokwe Mtu

Uvamizi wa maeneo ya hifadhi za misitu mkoani Katavi imetajwa kuwa chanzo cha mnyama  sokwe mtu kuendelea kupungua. Josephine Lupia na afisa misitu kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa amesema kuwa tabia ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu…

30 March 2022, 4:29 pm

RADI YAUWA NG’OMBE 28 KATAVI

KATAVI Ng’ombe 28 kati ya 52 waliokuwa pamoja wanatoka malishoni wa kaya tano tofauti kijiji cha Kabage kata ya Sibwesa Wilayani Tanganyika mkoa wa katavi zimekufa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua na upepo mkali. Hayo yameelezwa na…

30 March 2022, 1:16 pm

AJINYONGA BAADA YA KUMJERUHI MUMEWE

KATAVI.  Mkazi wa kitongoji cha Kamlenga, Kijiji cha Sibwesa wilayani Tanganyika, Mande Emanuel (30) amejinyonga baada ya kumjeruhi mumewe, Dotto Enos (35) kwa kumkata mapanga. Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amedhibitisha…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.