Jamii FM

Mtwara vijijini yanufaika na bilioni 4.74 za TPDC

26 November 2026, 06:57

Mbunge wa Jimbo Mtwara vijijini Mhe. Arif Premj akizungumza mbele ya wananchi waliokusanyika katika uwekaji wa jiwe la Msingi katika kongani la viwanda katika kijiji cha Maranje Mtwara vijijini(Picha na Mtwara RS)

TPDC imetoa zaidi ya shilingi bilioni 4.74 kupitia CSR kusaidia miradi ya maendeleo Mtwara Vijijini, huku mbunge wa jimbo hilo akiomba Serikali kuimarisha huduma za maji na kuwawezesha vijana kunufaika na gesi asilia

Na Musa Mtepa

Zaidi ya shilingi bilioni 4.74 zimetolewa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kupitia mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Mtwara Vijijini.

Akizungumza Novemba 13, 2026, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la kongani ya viwanda vya kuongeza thamani ya korosho katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Mji wa Nanyamba, Mbunge wa Jimbo hilo, Arif Premji, amesema wananchi wameanza kunufaika na uwekezaji wa gesi asilia kupitia miradi mbalimbali, hususan katika sekta ya afya.

Sauti ya Arif Premji, Mbunge wa Mtwara Vijijini

Aidha, Premji amemuomba Makamu wa Rais kuishinikiza Serikali kuhakikisha upatikanaji wa maji ya kutosha katika Jimbo la Mtwara vijijini, hususan maeneo ya ukanda wa bara, ili kumaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Sauti ya Arif Premji, Mbunge wa Mtwara Vijijini

Sambamba na hilo, ameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuwawezesha vijana wa Mtwara vijijini na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla kunufaika na rasilimali ya gesi asilia kupitia fursa za ufadhili wa masomo na uwezeshaji wa kiuchumi.

Sauti ya Arif Premji, Mbunge wa Mtwara Vijijini

Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Serikali inatekeleza miradi zaidi ya kumi ya maji katika Jimbo la Mtwara Vijijini, huku akieleza kuwa kutokana na ukubwa wa changamoto ya maji, Mkoa wa Mtwara umetengewa fedha maalumu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji kama eneo la dharura.

Sauti ya Jumaa Aweso, Waziri wa Maji

.