Jamii FM

Mtenga: Nitachangia mifuko 100 ya saruji bakwata

15 May 2021, 19:50 pm

Na Karim Faida.

Waislam katika wilaya ya Mtwara wametakiwa kuonesha jitihada na kushirikiana katika ujenzi wa ofisi ya bakwata ya wilaya hiyo ili kuwapa Imani wanaotaka kusaidia kwenye ujenzi huo ambao bado haujaanza kutokana na ukata wa pesa.

Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Mh Hassani Mtenga akizungumza wakati wa sherehe hizo

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Mh Hassani Mtenga wakati wa maadhimisho ya baraza la Eid lfitir jana Mei 14.

2021 ambapo kiwilaya yamefanyika katika kata ya Naliendele na kuhudhuliwa na viongozi na watu mbalimbali.Mh Mtenga ametoa ahadi ya kuchangia mifuko 100 ya saruji ili kuunga mkono juhudi hizo pamoja na kununua spika zitakazotumika na ofisi ya bakwata wilaya.

Waislam wakimsikiliza Mbunge wa Mtwara

Kwa upande wake Ustadhi Ismaili Ngome wa Madrasat Taqwa iliyopo kijiji cha Moma halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, amepongeza hatua ya Mbunge huyo kuahidi kuunga mkono ujenzi wa ofisi ya bakwata kwa kuwa itasaidia kurahisisha majukumu ya viongozi wake.

Maadhimisho hayo yaliyoanza saa 8:00 jioni yametoa mwanga kwa wazazi kuwapeleka watoto wao madrasa ili kujifunza elimu Ahera.