Bw. Jumbe Makoba
Jamii FM

TAKUKURU Mtwara yasaidia ukamilishaji wa miradi ya maendeleo

16 August 2023, 15:49 pm

Bw. Jumbe Makoba
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara Bw. Jumbe Makoba akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) ofisini kwake. Picha na Musa Mtepa

Na Musa Mtepa;

Taasisi ya kuzuia na kupambana  na Rushwa  TAKUKURU Mkoani Mtwara katika kipindi cha mwezi Aprili -Juni 2023 imefanikiwa kuokoa Miradi ya Maendeleo ambayo  awali ilikuwa kwenye mtanziko wa ukamilishaji kutokana dosari za Wazabuni katika utekelezaji wake.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Agost 16, 2023  Naibu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara Bw. Jumbe Makoba amesema kuwa  kwa ushirikiano na uongozi wa hospitali ya rufaa ha Ligula   wamewezesha ukamilishaji wa mradi wa Bwalo la kulia chakula na usimikqji wa mtambo wa kuchomea taka.

Aidha Bw Jumbe amesema kuwa TAKUKURU imewezesha mradi wa upuliziaji Dawa za kuua wadudu (Fumigation) ambapo mzabuni wa awali alilazimika kurejesha fedha kiasi cha shilingi 4,367,250/= na mzabuni mwingine kutafutwa na kuifanya kikamilifu katika maeneo yote ya hospitali.

Sambamba na hilo Bw Jumbe Makoba amesema wamewezesha kurejesha kiasi cha shilingi 11,228,000/=fedha za mradi wa uchimbaji wa kisima ambapo sasa mzabuni mpya anatafutwa  ili kuifanya kazi hiyo kwa uhakika katika mwaka wa fedha 2023/2024.

 Kwa upande wa taarifa za uchunguzi na Mashitaka Naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara amesema kwa kipindi cha April — juni wamepokea malalamiko 50,ambapo taarifa za Rushwa zikiwa 33 na zisizo za Rushwa 17  huku taarifa 33 kati ya hizo zikihusika kwenye Utawala 6, Elimu 6, Afya 6, Mapato 4, ujenzi 2, Polisi 2, Ardhi 2 na Maji 1 na majalada 9 ya uchunguzi yamekamili na mengine yakiwa katika hatua za  ufuatiliaji.