Jamii FM

TAKUKURU yaokoa Milioni 77.1 sekta ya Elimu Mtwara

27 April 2024, 15:51 pm

Kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Mashauri Elisante akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo 27/4/2024 (Picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wa uimarishaji umma ,tumeimarisha klabu za wapinga rushwa 70 zilizopo katika shule za Msingi, Sekondari na Vyuo ,Mikutano ya hadhara 68,Semina 37, maonesho 11 na utoaji wa Habari 3.

Na Musa Mtepa

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mtwara imeokoa kiasi cha shilingi 77,100,000 kwenye mradi wa sekta ya Elimu uliotekelezwa chini ya kiwango.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo tarehe 27/4/2024 kaimu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara  Mashauri Elisante Msolo amesema katika kipindi cha kuanzia Mwezi January hadi March,2024 walifanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ,matundu matatu ya vyoo na ununuzi wa madawati 45 katika shule ya Msingi Msinyasi iliyopo wilayani  Nanyumbu na kubaini mapungufu katika Mradi huo.

Sauti ya 1 Mashauri Elisante Msolo kaimu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara
Ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Mtwara (Picha na Musa Mtepa)

Pia kaimu mkuu wa TAKUKURU amesema kuwa katika kipindi cha Mwezi January /March walifanya ufuatiliaji wa miradi mingine 17 ya maendeleo  yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5.09  yote ikiwa katika sekta ya Elimu  ambapo katika miradi hiyo 14 sawa na asilimia 82.35  yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3.96 ilibainika kuwa na mapungufu.

Sauti ya 2 Mashauri Elisante Msolo kaimu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara

Aidha  Mashauri Elisante ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali katika mkoa wa Mtwara kwa kila mmoja kwa nafasi yake ,kuhakikisha anashiriki katika kuzuia vitendo vya rushwa kwenye maeneo ya utoaji wa huduma na ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Sauti ya 3 Mashauri Elisante Msolo kaimu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara