Jamii FM

Wananchi Mtwara washauriwa kuwa na utamaduni wa kupanda miti

21 April 2024, 16:26 pm

Mwonekano msitu na miti iliyopandwa (picha kwa hisani ya Mtandao)

Miti na misitu ina faida nyingi   kwa maisha ya binadamu ikiwa ni Pamoja na kuwa chanzo cha mvua,dawa ,chakula na ni chanzo cha bidhaa za ujenzi

Na Gregory Milanzi

Wananchi  wameshauriwa kuwa na utamaduni wa  upandaji wa miti ili kukabiliana na  mabadiliko ya tabia nchi Pamoja na urejeshwaji wa uoto wa asili uliopotea.

Hayo yamesemwa na afisa mazingira Mkoa wa Mtwara alipokuwa anazungumza na Jamii fm radio ambapo amesema kuwa wananchi hawana budi kuendelea na utunzaji wa misitu Pamoja na upandaji wa miti .

Aidha Masumbuko amesema kuwa  upandaji wa miti wananchi wanaweza kupanda miti yenye manufaa ikiwemo ya matunda  kama vile mikorosho ,mipapai ambayo inaweza kuwa sehemu ya kilimo na wakati mwingine ikitunza mazingira .

Sauti ya 1 Masumbuko Mtesigwa afisa mazingira mkoa wa Mtwara
Wanafunzi wa shule ya msingi ufukoni Manispaa ya Mtwara Mikindani wakipanda mti kwa ajili ya kutunza na kupendezesha eneo shule hiyo(picha na Musa Mtepa)

Akizungumzia mikakati ya ofis i ya mazingira mkoa wa Mtwara katika utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti amesema kuwa wanaendelea na uboreshaji na  utaratibu wa kuwa na klabu za wanafunzi mashuleni ili baadae wawe  msaada mkubwa wa kuelimisha jamii  juu ya utunzaji wa Mazingira.

Sauti ya 2 Masumbuko Mtesigwa afisa mazingira mkoa wa Mtwara
Wanafunzi wa shule ya msingi Ufukoni Manispaa ya Mtwara Mikindani wakiwa katika zoezi la upandaji wa miti(picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake afisa Muhifadhi Mwandamizi kutoka ofisi ya Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa wilaya ya Mtwara Peter Christopher Nguyeje ameelezea umuhimu wa uwepo wa miti na misitu katika Maisha ya binadamu kuwa ni Pamoja na upatikanaji wa dawa ,vyakula Pamoja na kusaidia kuzuia mmonyoko wa udongo.

Sauti ya 1 Peter Nguyeje afisa Muhifadhi Mwandamizi kutoka ofisi ya Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa wilaya ya Mtwara

Hata hivyo Peter Nguyeje amesema wamekuwa wakitumia njia mbalimbali za kukabiriana na athari za ukataji wa miti  ikiwa ni pamoja na   kutoa Elimu kwa Wananchi kupitia vyombo vya habari juu ya athari ya ukataji holela wa miti .

Sauti ya 2  Peter Nguyeje afisa Muhifadhi Mwandamizi kutoka ofisi ya Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa wilaya ya Mtwara

Shafii Mohamedi Linangwa ni mkazi wa mtaa wa Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani amesema kuwa ukataji wa miti  hovyo umekuwa ukileta athari kubwa kwa upande wa binadamu ikiwepo upungufu wa kiwango cha mvua .

Pia Shafii Linangwa ameiomba serikali kuona haja ya kupunguza bei gesi ya kupikia majumbani ili kuepusha ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa ambao umekuwa ukitumiwa na watanzania wengi kama nishati ya kupikia.

Sauti ya shafii Mohamedi Linangwa mwananchi mkazi wa mtaa wa Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani