Jamii FM

Kizito aibuka mshindi uchaguzi TCCIA

8 April 2021, 17:32 pm

Kizito Garnoma ameibuka mshindi kwa nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara, kilimo na Viwanda TCCIA mkoa wa Mtwara kwa miaka minne ijayo.

Kizito Garnoma akiwashukuru wanachama wa TCCIA kwa kumchagua

Kizito amechaguliwa kushika wadhifa huo leo katika ukumbi wa Tiffany Diamond Mtwara huku akishinda kwa kura 45 kati ya kura 91 za wajumbe wote.

Mwenyekiti huyo amewashinda wagombea wenzake wawili ikiwa ni pamoja na Bakari Mchila aliyepata kura 35 na Alex Chibuno aliyepata kura 9 huku kura 2 zikiharibika.

Akiongea na wanachama baada ya kuwekwa Rasmi katika nafasi hiyo ameahidi kufuata nyayo za mtangulizi wake Swallah Said Swallah huku akisisitiza kuwa atakuwa mshauri mzuri wa serikali kwa maslahi ya wanachama na Wananchi wa Mtwara.

Kwa upande wake Dkt Kafiliti ambae ni mwanachama wa TCCIA amemshauri Mwenyekiti huyo kuanza na swala la kuongeza mnyororo wa thamani kwenye zao la korosho pamoja na kutumia Bandari ya Mtwara katika kusafirisha korosho.

Dkt. Kafiriti akizungumza na Jamii fm

Nae Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Swallah Said Swallah amemtakia kila la kheri kiongozi huyo mpya atakayehudumu kwa miaka minne.