Jamii FM

BAKITA wawapiga msasa waandishi wa Habari

16 April 2021, 09:28 am

Waandishi wa habari mkoa wa Mtwara wamepokea mafunzo ya namna sahihi ya matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili kutoka Baraza La Kiswahili Tanzania (BAKITA).

Kaimu mtendaji mkuu wa Baraza la Kiswahili Tanzania Bi. Consolata Mushi

Mafunzo hayo yametolewa Aprili 15, 2021 na kaimu mtendaji mkuu wa Baraza la Kiswahili Tanzania Bi. Consolata Mushi katika ukumbi wa mkuu wa wilaya Mtwara mikindani

I

Bi. Consolata amewashukuru waandishi waliojitokeza katika kushiriki mafunzo hayo kwani bila wao mafunzo hayo si chochote.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara wakiwa kwenye mafunzo

Pamoja na hayo Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani Mtwara (MTPC) amewashukuru Baraza la kiswahili nchini kwa mafunzo hayo na ameomba kuwe na mwendelezo wa mafunzo na kongamano ili kuongeza ujuzi wa matumizi sahihi ya kiswahili kwa wanahabari.