Jamii FM

Nyumba yateketea kwa moto

21 May 2021, 15:05 pm

Na Karim Faida

Wananchi wa mtaa wa Mmingano kata ya Tandika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani hapa wameguswa na tukio la moto lililotokea Mapema Asubuhi ya leo ambapo nyumba ya Ndugu Sefu Bahili imeungua yote na hakuna kilichookolewa.

Bi hawa Hassani mkazi wa Mtaa wa mmingano

Akiongea na Jamii fm Radio katika eneo la tukio Bi hawa Hassani mkazi wa Mtaa huo amesema kutokana na hali ya Ndugu Bahili kiuchumi hawezi kupata tena makazi kama hayo kwa kuwa ana maisha ya kawaida na kuomba wadau wamsaidie kujenga nyumba nyingine.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mmingano Ndugu Abdallah Mussa

Nae Mwenyekiti wa mtaa huo wa Mmingano Ndugu Abdallah Mussa amesema tukio hilo limetokana na hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulianzia kwenye mita ya umeme ya nyumba hiyo.

Nyumba iliyoungua