Jamii FM

Mhe. Waziri Ndalichako awasili Mtwara

7 March 2023, 00:12 am

Waziri wa Nchi – Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Kanali Ahmed Abbas (Kulia). Picha na Mohamed Massanga

Na Mohamed Massanga

Waziri wa Nchi – Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewasili mkoani Mtwara leo Machi 6, 2023 kwa ziara ya siku mbili kwa lengo la kukagua maendeleo ya maandalizi ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Aprili 02, 2023.

Mhe. Prof. Ndalichako amepokelewa na viongozi wa mkoa wa Mtwara ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Kanali Ahmed Abbas huku imani na matarajio yake kuona Mkoa wa Mtwara ukifanya vizuri zaidi katika uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru kuupiku mkoa wa Njombe uliozindua mwaka jana.

Prof. Ndalichako ametembelea Uwanja wa Nangwanda sijaona na kugagua na kuona maendeleo ya shughuli za Maandalizi zinazofanywa katika uwanja huo kuelekea Uzinduzi wa mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa April 2, 2023.

Ziara ya Mhe Prof. Ndalichako itakamilika kesho kwa kutembelea na kukagua maenneo mengine pamoja na kwenda kuangalia mazoeozi ya vijana wa alaiki.