Jamii FM

Tuilinde Amani kwa nguvu

16 April 2021, 07:46 am

Wananchi wa Kijiji cha Ngorongoro kata ya Nanguruwe halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani hapa wameaswa kuendelea kuilinda amani kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Diwani wa kata ya Nanguruwe – Patrick Simwinga

Hayo yamesemwa jana April 14 2021 na Diwani wa kata ya Nanguruwe Mh Patrick Simwinga katika mkutano wa hadhara alioufanya kijijini hapo kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuilinda kwa gharama yoyote amani hii tuliyonayo kwani ikitoweka ni vigumu kuipata tena.

Mwenyekiti wa Kijiji – Saidi Ngulyungu

Awali akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu Saidi Ngulyungu amewataka wananchi kutozurura bila sababu majira ya usiku ili kuwapa nafasi Polisi Jamii na sungusungu wa kijiji hicho kufanya kazi yao vizuri ya kulinda kijiji hicho kilichopo umbali wa km 5 kutoka Makao makuu ya kata yalipo.

Viongozi mbalimbali wa mkoa huu wa Mtwara, wamekuwa wakihamasisha amani na wananchi Kuweka maslahi ya Taifa mbele ikizingatiwa kwamba mkoa wetu tumepakana na Nchi ya Msumbiji ambako hali ya amani sio nzuri sana kwa sasa.