Mwanafunzi mjamzito
Jamii FM

Watoto 8,172 wapata ujauzizo mkoani Mtwara

8 March 2023, 23:06 pm

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmedi Abbas akihutubia wananchi katika maadhimisho yasiku ya Mwanamke Duniani katika wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara. Picha na Juma Khomeni

Na Mohamed Massanga

Watoto zaidi ya 8,172 wenye umri wa kuanzia miaka 10 hadi 19, wameripotiwa kupata Mimba Mkoani Mtwara kuanzia mwezi Januari hadi Disemba mwaka 2022.

Akizungumza leo Machi 8, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwanamke Dunuani katika Halmashauri ya Wilaya Tandahimba, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas, amesema mkoa bado unakabiliwa na tatizo la mimba za utotoni, ambapo zaidi ya asilimia 19.4 ya wajawazito waliopata huduma katika vituo vya afya ndani ya halmashauri ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 19.

Mhe Kanali Abbas amesema kwa takwimu hizo utaona kwa kiwango gani Mimba za utotoni ni sehemu ya tatizo katika mkoa mkoa wa Mtwara na kuwataka wananchi kukumbuka kuwa Mimba za utotoni huathiri afya, elimu na haki za mtoto wa kike.

Machi 8 Kila mwaka Dunia huadhimisha Siku ya Wanawake Duniani na kwa mwaka huu 2023 kauli mbiu ni: Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia, chachu ya kuleta usawa wa kijinsia.