Jamii FM

Wakulima washauriwa kufuatilia utabiri wa hali ya hewa ya hewa wa kilimo

2 December 2022, 17:32 pm

Na Mussa Mtepa

Wakulima wameshauriwa kuacha kilimo cha mazoea na kuanza kufuata taratibu zinazoelekezwa na wataalamu wa kilimo.

Akizungumza na Jamii fm Radio afisa utabiri wa hali ya hewa kutoka kituo cha utafiti na kilimo TARI Naliendele Omari Rashidi Kahoki amesema kuwa kwa miaka ya hivi karibu kumekuwa na mvua za chini ya wastani  na wastani ambazo kiuhalisia ni mvua ndogo  ambazo wakulima wanatakiwa kuzitumia ipasavyo  na kufuata kile wataalamu wa hali ya hewa na kilimo wanacho waelekeza.