Picha ya nyezo za mahakamani
Jamii FM

Kipindi: Watanzania wengi wanaishi kwenye dhana ya ndoa na sio Ndoa

3 August 2023, 14:21 pm

Na Musa Mtepa

Akizungumza katika kipindi maalumu kinachorushwa na jamii FM redio cha tarehe 25/07/2023,Hakimu Mkazi kutoka mahakama ya Mwanzo Mkoani Mtwara Ndugu Alex Robert amesema baada ya ndoa kufungwa inapaswa kusajiriwa katika taasisi  ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini yaani RITA.

kifungu cha 160 cha sheria ya ndoa sura ya 29 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 inasema watu wakiishi chini ya paa moja kwa kipindi cha miaka miwili wanawaweza kutambulika kama wanandoa (dhana ya ndoa). picha kwa msaada wa mtandao

Ndoa lazima isajiriwe na kupata cheti kutoka RITA na vyeti vinavyotakiwa vitolewe ni vya serikali,  Watu wengi wamefunga ndoa na haijasajiriwa na wengine wanafunga ndoa bila kupata vyeti kitu ambacho kinapeleka watu kuishi katika dhana ya ndoa badala ya ndoa kwa mujibu wa sheria.

Hakimu Mkazi Alex Robert amesema hakuna mahali popote ambapo sheria inatambua kuwa watu wakiishi pamoja mwenza wake kwa miezi sita au mitatu ni mke au mume wa ndoa sio kweli na hakuna sheria inayozungumzia suala hilo, katika kifungu cha 160 cha sheria ya ndoa sura ya 29 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 inasema watu wakiishi chini ya paa moja angalau kwa kipindi cha miaka miwili wanaweza kutambulika kuishi kwenye dhana ya ndoa.

Sikiliza kipindi hiki ili upate elimu kuhusu masuala ya ndoa na taraka, Bonyeza hapa