Jamii FM

Madiwani Manispaa ya Mtwara watembelea miradi ya Maji MTUWASA

17 February 2021, 09:59 am

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani wamefanya ziara ya kuangalia miradi na vyanzo vya maji vya Mamlaka ya Maji safi na maji taka mjini Mtwara (MTUWASA) kwa lengo la kujifunza na kuona namna ya ufanisi wa kazi wa mamlaka hiyo.

Wadiwani wakiangalia moja ya miundombinu ya maji

Akizungumza kwa niaba ya madiwani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile, amewapongeza MTUWASA kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa wananchi na kuwaomba waongeze wigo wa kuwafikia wananchi wote wanaohitaji huduma ya maji safi na salama.

Madiwani hao watembelea vyanzo vya maji vya Mtawanya, Mjimwema na Mchuchu Mikindani na kujionea kazi zinazofanyika.

Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa miundombinu ya maji